Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Ihefu weka niweke

F93D9F29 414A 4D0B BF8B A5519CCD8780.jpeg Wachezaji wa Kikosi cha Ihefu

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ihefu ikiwakaribisha Simba, mashabiki wa timu hizo wametunishiana misuli kila upande ukitamba chama lake kufanya kweli.

Timu hizo zinakutana ikiwa ni mchezo wa sita katika mashindano, ambapo Simba inajivunia rekodi ya kushinda michezo yote.

Hata hivyo Ihefu nao wamekuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi kuu haswa wanapokuwa uwanja wao Highland Estate Mbarali kutokana na matokeo mazuri waliyopata hivi karibuni.

Timu hiyo ambayo haikuwa na mwanzo mzuri ndio inashikilia rekodi ya kuisimamisha Yanga ambayo ilicheza zaidi ya mechi 40 bila kupoteza ilipolala mabao 2-1.

Haikuishia hapo kwani vijana hao wa Mbogo Maji waliifanyia mbaya Azam walipoikanda bao 1-0 huku Singida Big Stars wakiambulia sare ya 1-1 na leo inakamilisha hesabu kwa timu nne za juu dhidi ya Wekundu hao.

Petro Mwamanya shabiki wa Ihefu amesema licha ya kupoteza mchezo uliopita wa kombe la shirikisho (ASFC) kwa mabao 5-1 leo wanaenda kulipa kisasi.

"Tuliumia na matokeo hayo, lakini hatukufa moyo wameyakanyaga, kuvuka daraja tu tayari wameshaisha, hawa ni wetu mabao mawili yanawahusu" amesema Mwamanya.

Naye Moses Richard shabiki wa Simba tawi la Uyole amesema licha ya kubebwa na rekodi lakini ushindi leo uko palepale akimtaja Straika, Jean Baleke kupeleka shangwe.

"Tangu kuja kwa Kocha Robertinho amekuwa na kikosi cha kwanza huku kikionesha uwezo naamini leo tunashinda" amesema Richard.

Chanzo: Mwanaspoti