Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Hatukuamini kama tungempiga 3-0 Azam FC

Ngoma Fredy .jpeg Simba: Hatukuamini kama tungempiga 3-0 Azam FC

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa walijua kama wangemfunga Azam Fc katika mchezo wa jana lakini hawakujua iwapo wangemfunga mabao mengi kiasi kile kutokana na ubora walio nao timu hiyo.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Tumempasua Azam tuna furaha kubwa mno leo. Azam ni moja kati ya timu bora, nzuri na ngumu sana kwenye ligi yetu. Japo walianza vibaya ligi lakini sasa hivi wamejipata wanapata matokeo.

“Sisi tulijua hata iwejelazima tumfunge Azam ila hatukujua kama tungempiga tatu. Tulidhani tungemfunga bao moja au mbili, kumfunga bao tatu hatukuwa tumejiandaa ndiyo maana unamuona hata Duchu wakati anafunga bao la tatu alishangilia nusura afe.

“Hii ndiyo Simba ambayo tunaitaka, hapo katikati hatukuwa na matokeo mazuri lakini tumeitengeneza haraka haraka na kurejea kwenye makali yetu,” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba Sc ni dhidi ya Kagera Sugar FC unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Mei 12, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live