Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Azam wapigana vikumbo kwa Kibwana Shomari

Kibwana Tiziii Kibwana Shomari

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu vya Azam na Simba vimetajwa kuonesha uhitaji wa kuipata huduma ya Mlinzi wa kulia Kibwana Shomari ambaye ana maliza kandarasi yake mwisho wa msimu huu na waajiri wake ila hawajafikia mahitaji anayohitaji Mlinzi huyo.

Inaelezwa kuwa, Klabu ya Azam ndio wa kwanza kuonesha uhitaji wa Mlinzi huyo wa Klabu ya Yanga lakini ada ya usajili anayohitaji imekuwa kikwazo kwao.

Simba Sc pia walionyesha kuihitaji huduma ya mlinzi huyo huyo pia ila nao wakakwama kwenye ada ya usajili japo inafahamika Simba Sc wamepanga kurudi tena kwa Mlinzi huyo anayesifika kuwa kizingiti kwa mawinga wote hatari Tanzania.

Muda wowote kuanzia sasa, Uongozi wa Yanga Utaketi mezani na Mlinzi huyo ili Kuongeza kandarasi mpya, japo bado haijafahamika kama Young Africans wamemuandalia kandarasi ya Miaka Miwili ama Mitatu ila nafahamu kuwa Wanaelekea kuketi nae Mezani.

Kipaumbele cha Kibwana Shomari ni kama ilivyo Klabu ya Yanga ni kuendelea kusalia klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live