Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Arta Solar 7 ngoma ngumu

Simba SC X Art Solar Simba, Arta Solar 7 ngoma ngumu

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 45 za kipindi cha kwanza za mchezo wa kirafiki wa kimataifa zimemalizika kwenye Uwanja wa Uhuru kwa wenyeji Simba kutoka suluhu ya 0-0 na AS Arta Sola 7 kutoka Djibouti.

Mchezo huo wa kujipima nguvu kwa timu zote ulianza kwa Simba kulishambuliaji lango la wapinzani wao huku kiungo mshambuliaji, Moses Phiri akionekana mwiba kwa Wadjibouti.

Phiri amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo huu tofauti na ilivyokuwa mechi iliyopita dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambapo Kocha Zoran Maki alianza na Mserbia, Dejan Georgijevic kwenye eneo hilo aliyeanzia benchi leo.

Phiri ambaye amekuwa tishio dakika hizi 45, amesaidiwa na viungo wenzake washambuliaji, Peter Banda, Nelson Okwa na Augustine Okrah.

AS Arta Solar ambao ndio mabingwa wa Ligi ya Djibouti wamekuwa kivutio kikubwa nchini kutokana na uwepo wa mastaa wakubwa, Salomon Kalou aliyewika na Chelsea na Alex Song aliyekipiga Arsenal zote za England.

Eneo la kiungo la Simba linaloongozwa na Sadio Kanoute, Nassor Kapama na Victor Akpan limeonekana kuwatesa wapinzani wao huku wakitumia zaidi mashambulizi kupitia pembeni ambapo hata hivyo hayakuweza kuleta matunda.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatamatika sio wenyeji Simba wala Arta Sola 7 iliyoliona lango la mwenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live