Dakika 90 zimekamilika katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam huku mchezo wa mkondo wa kwanza African Football League ukimalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Sio mwenyeji Simba SC wala Al Ahly waliofanikiwa kuondoka na ushindi katika mchezo huo mgumu ulioshuhudiwa na viongozi wa juu wa Soka ulimwenguni.
wageni Al Ahly ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Reda Slim mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika wageni Al Ahly walikwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa uongozi wa bao 1-0.
Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Luis Miquissone na mzamiru Yassin kisha nnafasi zao kuchukuliwa na Sadio Kanoute na Jean Baleke.
Mabadiliko hayo mawili yaliongeza ari kwa simba kwani dakika ya 53 walipata bao la kusawazisha kupitia kwa kibu Denis akimaliza pasi safi ya Clatous Chama, kisha dakika ya 60 wakaongeza bao la pili kupitia kwa Sadio Kanoute akimaliza mpira wa kona kutoka ka Saido Ntibazonkiza.
Dakika ya 63 Al Ahly walirudi mchezoni na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kahraba na kuweka mzani sawa.
Mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo kuacha nafasi wazi ya kila mmoja kusonga hatua inayofuata pindi watakapokutana katika Robo Fainali ya mkondo wa pili Oktoba 24 nchini Misri