Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silva, Guardiola watofautiana Manchester City

Bernado Silva X Pep Guardiola Silva, Guardiola watofautiana Manchester City

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuenea kwa tetesi kwamba kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva anataka kuondoka mwisho wa msimu huu, kocha Pep Guardiola amesema ana matumaini makubwa staa huyo ataendelea kuwepo kwa muda mrefu.

Silva ambaye alijiunga na Man City mwaka 2017 akitokea Monaco, yupo kwenye rada za Barcelona na baadhi ya timu za Saudi Arabia.

LICHA ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa muda mrefu, beki wa Lille Leny Yoro amewaambia wawakilishi wake kwamba anatamani zaidi kutua Real Madrid na sio Man United.

Kwa mujibu wa Marca, Madrid imewasiliana na wakala wa Leny na kumwambia kwamba wanamhitaji mchezaji wake. Msimu huu Leny amecheza mechi 44 za michuano yote.

CELTIC inafanya mazungumzo na Newcastle kwa ajili ya kuipata saini ya golikipa wa timu hiyo Martin Dubravka, katika dirisha hili, inaelezwa. Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Record Newcastle ipo tayari kumwachia Martin na tayari imeshaanza kutafuta kipa mpya atakayekwenda kuziba pengo lake. Msimu uliomalizika alicheza mechi 30 za michuano yote.

TAYARI mabosi wa Bayern Munich wameshafikia makubaliano na wawakilishi wa beki wa kati wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah ambaye imepanga kumsainisha mkataba wa miaka mitano utakaodumu hadi mwaka 2029.

Tayari beki huyu amewaambia mabosi wa Leverkusen kwamba anataka kuondoka. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025

KOCHA wa Tottenham, Ange Postecoglou ameidhinisha mchakato wa kuachana na kiungo wa timu hiyo, Tanguy Ndombele, 27, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Galatasaray.

Ndombele ambaye msimu uliopita alicheza mechi 26 za michuano yote akiwa na Galatasaray, mkataba wake unamalizika mwaka 2025. Katika mkataba wake wa mkopo kuna kipengele kinachowapa nafasi Galatasaray ya kumsajili mazima.

REAL Betis imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Tottenham na Argentina, Giovani Lo Celso katika dirisha hili. Lo Celso ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 24 za michuano yote, anataka kuondoka Spurs kwa ajili ya kutafuta changamoto sehemu nyingine kwani hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.

IKIWA ni siku kadhaa tangu kiungo wa Everton na Ubelgiji, Amadou Onana aweke wazi kwamba anataka kujiunga na moja kati ya timu kubwa barani Ulaya, Arsenal na Chelsea zimetajwa kutaka kumsajili. Everton inahitaji walau Pauni 50 milioni kwa ajili ya kumuuza fundi huyu ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka.

Chanzo: Mwanaspoti