Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sillah ni suala la muda tu

G Sillah Sillah ni suala la muda tu

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Azam FC, Gibril Sillah anaendelea vizuri baada ya kuumia nyonga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania uliomalizika kwa matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam kushinda 2-1, Desemba 11.

Daktari wa Azam, Mbaruku Mlinga alisema maendeleo ya nyota huyo ni mazuri na majeraha yake sio siriasi sana hivyo mashabiki wa kikosi hicho wamtegemee kumuona uwanjani siku za karibuni.

“Jana na juzi tulimfanyia vipimo na kugundua jeraha sio kubwa sana hivyo ni matumaini yetu mchezo wetu wa keshokutwa wa Kombe la FA dhidi ya Alliance anaweza akawa fiti kucheza ingawa itategemea tu na matakwa ya benchi la ufundi,” alisema.

Mlinga aliongeza dawati la matibabu wanapambana kwa hali na mali ili kuhakikisha wachezaji wote waliokuwa na majeraha wanarejea kwa wakati katika hali zao za kawaida ili kuifanya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri.

“Ukiangalia mwenendo wa timu yetu kwa sasa tunataka kuona kila mchezaji anakuwa kwenye utimamu wa mwili kwa asilimia 100 hivyo tunaendela kupambana kwa ajili ya kuwarejesha katika hali ya kawaida kwa manufaa ya kikosi chetu.”

Winga huyo raia wa Gambia aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu akitokea Raja Casablanca ya Morocco amekuwa na kiwango bora hadi sasa kwani amefunga mabao matatu ya Ligi Kuu Bara huku akiasisti mabao matatu.

Chanzo: Mwanaspoti