Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sillah aanza kujipata Ligi Kuu

G Sillah Sillah aanza kujipata Ligi Kuu

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota mpya wa Azam FC, Gibril Sillah raia wa Gambia, ameanza kujipata Ligi Kuu Bara kufuatia kupachika mabao katika michezo miwili mfulilizo dhidi ya Yanga na Mashujaa ya Kigoma, jambo ambalo anadai linamfanya kutaka kufanya makubwa zaidi.

Winga huyo wa zamani wa Raja Casablanca, alisema awali alikuwa na wakati mgumu kuzoeana na wachezaji wenzake huku akijitahidi kuendana na ushindani uliopo kwenye soka la Tanzania ambalo ni tofauti na Morocco ambako ametokea.

“Ligi ya Tanzania ni ngumu kwa sababu ni nadra mchezaji kupata nafasi ya kutosha ya kuwa na mpira mguuni, mabeki wengi wanacheza soka la nguvu hivyo inaweza kukufanya mara nyingi kushindwa kufanikisha kile ambacho unakuwa unalenga lakini hilo kwangu sio tatizo na kwa sasa najiona kuzoea,” alisema.

Sillah mwenye uwezo mzuri zaidi wa kutumia mguu wa kushoto, aliongea kwa kusema; “Natamani kuendelea kufunga mabao zaidi na zaidi ili kuisaidia timu yangu kutwaa ubingwa naamini bado tuna nafasi ya kupigania hilo.”

Mgambia huyo na wachezaji wenzake wana kibarua kingine leo Jumamosi cha kupigania matokeo mbele ya Ihefu kwenye Uwanja wa Highland Estate huko Mbeya.

Kocha wa Azam FC, Youssouph Dabo alisema; “Mechi itakuwa ngumu kama ilivyokuwa Kigoma lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri na kusogea kwenye nafasi za juu.”

Kwa upande wake kocha wa Ihefu, Moses Basena alisema; “Pamoja na ubora wao tumetafuta namna nzuri ambayo tunaweza kukabiliana nao.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: