Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sillah, Dube wampoteza Mbombo ndani ya Azam

Idris Mbombo Amkosha Sillah, Dube wampoteza Mbombo ndani ya Azam

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita mpya imeibuka kwa washambuliaji wa Azam FC, Djibril Sillah na Prince Dube huku ufalme wa Idris Mbombo ukizimwa kabisa kutokana na kushindwa kutupia bao hata moja kwenye mechi sita za kirafiki walizocheza hadi sasa.

Katika michezo hiyo Azam imefanikiwa kushinda michezo minne ambapo waliifunga Al Hilal mabao (3-0), Us Monastir (2-1), Bandar (2-0), KMKM (4-0) na kupoteza nmicghezo miwili dhidi ya Esperance (3-0), Stade Tunis (3-1) mchezo uliovunjika dakika ya 62.

Katika michezo hiyo sita waliyocheza Azam Fc wamefunga mabao 12 na kufungwa mabao sita huku Mbombo akishindwa kutupia bao hata mioja wakati Sillah ametupia mabao matatu Dube mawili.

Akizungumza Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssoph Dabo ambao wapo Tanga tayari kwaajili ya mechi ya leo dhidi ya Yanga alisema wanaendelea kuboresha mbinu za ushambuliaji lengo ni kuwafunga wapinzani.

“Kadri muda unavyosonga napata mabadiliko kwenye safu yangu ya ushambuliaji idadi ya mabao inaongezeka na sio kila mshambuliaji kazi yake ni kufunga anaweza akamtengenezea nafasi mchezaji mwenzake kubwa ni matokeo ya ushindi bila kujali nani kafunga;

“Ni mapema sana kumsifia nani jicho la kuona lango la wapinzani naamini wachezaji waliopo wote ni wazuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live