Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silaha za Pablo hizi hapa

Pablo Martin 5 3 22 Pablo Franco Martin

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Pablo Franco mara alipotua nchini na kutambulishwa na klabu ya Simba, kuna baadhi ya wadau walimponda, lakini ghafla jamaa amekuwa mtamu na nyota na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Mussa Mgosi kuanika kinachombeba.

Mgosi aliyecheza kwa mafanikio Msimbazi, alisema anaamini kocha huyo hunda atavunja rekodi za makocha wageni waliowahi kupita hapa nchini kutokana na mwenendo wake pamoja na matokeo wanayowapata Simba.

Akizungumza alisema alichobaini kinachombeba Pablo ni elimu kubwa ya soka aliyonayo, jambo linalomfanya kuwa na mbinu mbadala wa kutatua changamoto za nje na ndani ya uwanja zinazoikabili kikosi chake.

“Ni kocha anayetumia akili nyingi kufanya kazi zake na kuyatekeleza kwa umakini mkubwa ukilinganisha na makocha wengine, pia anasimamia misimamo yake ambao imekuwa ikimpa matokeo mazuri bila ya wengi kutarajia,” alisema.

“Tangu atue na kuiongoza Simba, nimegundua hilo na pia natarajia kuona Simba ikifanya makubwa zaidi ikiwa chini ya Kocha huyo ila jambo kubwa ni kumpatia muda na kumuamini pasipoingilia kazi atazidi kuipasha timu,” aliongeza Mgosi.

Alisema licha ya Simba kuanza ovyo ligi, lakini Pablo ameibadilisha timu na kubwa ni uwezo wa kukaa na wachezaji na kuzungumza nao na kuwarejeshea morali yao, kitu ambacho kinambeba sasa.

“Kadri siku zinavyokwenda timu inazidi kuimarika tofauti na alivyoikikuta, jambo hilo linatoa fundisho kwa makocha wengine pale wanapopewa timu zenye presha kama ilivyo kwa Simba, kufanya kazi kwa uwezo walionao.”

Kauli hizo zimeungwa mkono na staa mwingine wa Msimbazi aliyewahi kukipiga pia Pamba, George Masatu aliyesema; “Ana ubunifu mkubwa na akiendelea kupata muda zaidi basi sitoshangaa akifanya makubwa.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz