Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku zinahesabika kwa Moises Calcedo

Mioses Caicedo CFC.jpeg Moses Caicedo

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Suala la uhamisho wa Kiungo kutoka Ecuador Moises Calcedo huenda likafikia mwisho hivi karibuni baada ya Kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi kutoa kauli nzito.

Caicedo alikosekana katika mchezo wa Seagulls wa kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano, ambao ulimallzika kwa sare ya bao 1-1, kukosekana kwake kulikuwa kama nafasi kwa Chelsea.

Alipoulizwa kuhusu kuingo huyo, De Zerbl alisema: “Sijui kama atakuwa mazoezini leo. Kama Moises ataondoka, tutatafuta mchezaji mwingine muhimu.

“Na kama Moises atabaki, nitakuwa na furaha, timu pia, pamoja na klabu. Lakini si tatizo langu sasa.

“Kama Molses ataondoka, tutasajill mchezaji mwingine. Sisi ni Brighton, na sera yetu ipo wazi kwamba kila mwisho wa msimu kutakuwa na wachezali wanaondoka. Hilo ni kama lililotokea kwa (Alexis) Mac Allister na (Levi) Colwill”

Chanzo: Dar24