Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku ya lawama.. Ni mchezaji yupi unatamani kumuona akisajiliwa na timu yako?

Epl Pic Januari 31 ndio siku ya mwisho ya dirisha la usajili Ligi tano kubwa Ulaya

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Muda wa lawama. Leo, Januari 31 ndio siku ya mwisho ya dirisha la usajili nchini England, Ufaransa, Hispania, Ujerumani na Italia.

Siku kama ya leo wataalamu wa mambo wanasema ndio umafya huwa unahusika kwenye madili mbali mbali na viongozi wa timu husika ili kuhakikisha wanapata kile wanachohitaji.

Licha ya dirisha kuwa linakwenda kufungwa leo lakini bado kuna madili yanayoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kukamilika kwa wachezaji husika kutoka walipo sasa kwenda timu nyingine katika dakika za mwisho za dirisha hili.

Mchezaji wa kwanza ambaye anaweza akaondoka kwenye timu aliyopo kabla ya dirisha kufungwa ni Donny van de Beek ambaye anahusishwa sana kwenye rada za Everton na Crystal Palace na timu inayoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsainisha ni Everton. Van de Beek anaweza akajiunga na wababe hao kwa mkopo wa nusu msimu.

Pia, picha mbali mbali jana ziliwaonyesha marafiki wawili kutoka Real Sociedad Adnan Januzaj na Alexander Isak wakiwa Jijini London na taarifa zinadai mafundi hao wapo nchini humo kwa ajili ya uhamisho.

Hakuna uhakika ni timu gani Januzaj anaweza akajiunga nayo lakini kwa upande wa Isak anaonekana kuwa na asilimia kubwa za kutua Arsenal kwenda kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji na Arsenal imeripotiwa kutaka kumsainisha kwa sababu imeikosa saini ya Dusan Vlahovic aliyejiunga na Juventus.

Tayari kumekuwa na vikao kadhaa baina ya wawakilishi wa Barcelona na wale wa kiungo wao Ousmane Dembele juu ya kujadili hatma ya staa huyo na taarifa za ndani zinadai uamuzi ulioafikiwa ni kwamba staa huyo atafutiwe timu ya kujiunga nayo katika dirisha hili.

Wawakilishi wa staa huyo wameonekana nchini England kwa ajili ya kujadili suala la uhamisho wa staa huyo hivyo kuna uwezekano mkubwa kabla ya dirisha kufungwa akawa amekamilisha dili la kutua England ambako timu inayoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili ni Newcastle United.

West Ham tayari imeshaweka Pauni 50 milioni mezani kwa Leeds United na inasikilizia kama ofa hiyo itakubaliwa ili kuipata huduma ya kiungo Kalvin Phillips, kama dili hilo litafanikiwa usajili huo pia utakuwa wa siku ya mwisho ya usajili.

Licha ya ukweli kwamba kocha Jurgen Klopp anatamani sana kuendelea kuwa na Divock Origi kwenye kikosi chake lakini taarifa za ndani zimefichua kwamba mabosi wa timu hiyo wana machaguo mawili juu ya straika huyo.

Moja ni kukubali kuchukua pesa kutoka kwa timu zinazomuhitaji katika dirisha hili na kutumia pesa hizo katika usajili wa Luis Diaz ambao kila kitu kipo sawa.

Chaguo jingine ni kumuacha akae hadi mwisho wa msimu kisha aondoke bure ikiwa atagoma kusaini mkataba mpya katika dirisha hili.

Ikiwa Liverpool itakuwa tayari kuchukua pesa basi staa huyu naye ataungana na wachezaji wengine wanaotarajiwa kusajiliwa katika dirisha hili.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya dili la Pierre Emerick Aubameyang na Ousmane Dembele ambapo ripoti zinadai Barcelona imeshafanya makubaliano na wawakilishi wa Aubameyang ili kumsajili kwa mkopo wa nusu msimu lakini dili hilo halitakamilika hadi Barca imuondoe Dembele kikosini.

Hivyo kuna asilimia zaidi ya 70 ikiwa dili la Dembele kutua England litakamilika basi na dili la Auba kutua Hispania nalo litakamilika.

Tayari Antony Martial ameshachukunja mkeka wake na ameenda kujaribu bahati nchini Hispania kwa kujiunga na Sevilla kwa mkopo. Mchezaji mwingine anayeonekana kwamba huenda akafuata nyayo zake ni Jesse Lingard kwa sababu mastaa hao wote hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Lingard amekuwa akiwindwa na timu nyingi ndani na nje ya England ingawa timu zinazopewa nafasi ya kuwa naye ni West Ham na Tottenham.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz