Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane amefikia makubaliano ya kuwa kocha mkuu wa miamba wa Ligue 1, Olympique de Marseille.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa nje ya ukocha wa soka tangu 2021, lakini mustakabali wake umebaki kuwa suala la uvumi.
Ndoto ya Zidane imekuwa ni kupata kazi ya ukocha katika timu ya taifa ya Ufaransa, lakini hatua hiyo haikutimia.
Mshindi huyo wa mfululizo wa Ligi ya Mabingwa sasa yuko tayari kuchukua mikoba ya Les Phoceens, lakini ripoti hiyo inaongeza kuwa hatua hiyo itawezekana tu ikiwa Saudi Arabia itakamilisha kutwaa klabu hiyo ya Ufaransa.
Zidane ana kibali cha kuwa msimamizi wa kusajili na kutumia takriban euro milioni 300 kama bajeti ya uhamisho ikiwa atahamia Velodrome.
Hata hivyo, kizingiti kikubwa kitakuwa kumshawishi mmiliki wa Marseille, Frank McCourt, ambaye amepinga kuuzwa kwa klabu hiyo kwa muda mrefu.
Les Phoceens watafurahi kusikia juu ya nia ya Zidane kufundisha klabu, kwani wamekosa meneja mwenye DNA na klabu hiyo kwa miaka mingi.
Huku ukiritimba wa Paris Saint-Germain katika kilele cha Ligue 1 ukidumu kwa muongo mmoja, umiliki unaoungwa mkono na Saudia na meneja wa daraja la juu kama Zidane ndicho kitu ambacho Marseille wanahitaji ili kuwa kinara na kushinda mataji zaidi.
Les Phoceens wameanza msimu mpya kwa misukosuko, huku Marcelino akiachia nafasi ya ukocha mkuu baada ya mechi saba tu baada ya kupoteza imani na mashabiki.
Miamba hao wa Ligue 1 hivi majuzi walimteua kocha wa zamani wa Valencia, Gennaro Gattuso kuwa meneja wao mpya lakini tayari kuna kuna taarifa kwamba uongozi umeamua kumpa umeneja Zidane.