Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku 6 ngumu JKT Queens Caf

JKT Quuens Mabingwa.jpeg Siku 6 ngumu JKT Queens Caf

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake yalianzishwa rasmi mwaka 2021 yakishirikisha timu nane kutoka kanda tofauti za soka Afrika.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, JKT Queens ina saa 144 za kuifikia rekodi ya Simba Queens itakapokuwa huko Ivory Coast mwezi ujao kushiriki mashindano hayo.

Rekodi ambayo inaweza kuivunja ni ya kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo bingwa wake anapata kitita cha Dola 400,000.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo iliyotolewa jana na Shirkisho la Soka Afrika (Caf), JKT Queens imepangiwa mechi tatu za kundi A ndani ya siku sita na ikifanya vizuri itaingia nusu fainali.

Wawakilishi hao wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati itarusha karata yao ya kwanza Novemba 5, kwa kuikabili Mamelodi Sundowns na itapumzika kwa siku mbili kisha Novemba 8 kucheza na wenyeji Athletico Abidjan.

Karata ya mwisho ya JKT Queens katika hatua ya makundi ni Novemba 11 itakapokabiliana na wawakilishi wa Morocco, SC Casablanca.

Kama itafanikiwa kumaliza nafasi mbili za juu kwenye kundi lao, JKT Queens itacheza mechi ya nusu fainali Novemba 15 na fainali ya mashindano hayo imepangwa kuchezwa Novemba 19.

Timu mbili tofauti zimewahi kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ambazo ni Mamelodi Sundowns iliyokuwa ya kwanza kutwaa ubingwa huo, huku AS FAR ikibeba msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live