Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikia hili senema la Labota aliyeitosa Yanga, atua Bongo kimya kimya

Manu Labota Bola Manu Labota aitosa Yanga

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukisikia umafia, ndio huu. Yanga ilikuwa ikimpigia hesabu winga Mkongomani, Manu Labota Bola, lakini kabla haijamalizana naye, dili likatibuka na jamaa akaibukia Singida Fountain Gate.

Mabosi wa Yanga wakasikitika kwa kumkosa mchezaji huyo na kuendelea na yao, lakini wakati kila mmoja akiamini Labota keshatua Singida kwenda kuliamsha mambo yamebadilika baada ya mchezaji huyo kutua Ihefu kama masihara vile.

Ipo hivi. Winga huyo tayari yupo nchini tangu juzi, lakini akiwa ni mchezaji wa Ihefu iliyopokutisha baadhi ya mastaa iliyokuwa nao kutokana kilichoelezwa timu ipo mbioni kuuzwa kwa mmoja vigogo nchini.

Wachezaji wengi wa timu hiyo wameomba kuondoka kwa hiyari yao, huku wengine wakiachwa kimya kimya kupitia dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa Jumatatu, huku mmoja ya wachezaji wapya alitua ili kuimarisha kikosi hicho akiwa ni Labota.

Kwa mujibu wa chanzo changu makini kilicho ndani ya Ihefu FC, winga huyo wamemnyakua muda mchache baada ya kutua Dar es Salaam na kumficha kwenye moja ya hoteli iliyopo jijini na tayari amesainishwa mkataba wa miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live