Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikia hii ya Neymar kumhusu Mbappe

Neymar X Mbappe Sikia hii ya Neymar kumhusu Mbappe

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Umesikia hii? Mwandishi wa habari Mfaransa amedai supastaa Neymar amewaandikia meseji wachezaji wa Kibrazili kwenye kikosi cha Real Madrid akiwaambia kucheza timu moja na Kylian Mbappe ni janga.

Mbappe alijiunga na Los Blancos kwa uhamisho wa bure akitokea Paris Saint-Germain kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi na tangu muda huo amefunga mabao manne kwenye mechi sita alizocheza akiwa na timu yake mpya.

Mbappe alikuwa akichukuliwa kama mfalme huko Paris, ambako alishinda mataji sita na kufunga mabao 256 katika misimu saba. Hadhi aliyopewa Mbappe kwenye kikosi cha PSG ilimfanya atibuane mara nyingi na mchezaji mwenzake wa zamani, Neymar.

Nahodha wa Brazil, Neymar alijiunga na PSG, Agosti 2017 kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya Pauni 198 milioni. Lakini, hadhi yake ilipokwa haraka baada ya Mbappe kujiunga na PSG kwa mkopo kabla ya kubebwa jumla kwa ada ya Pauni 166 milioni.

Kwa nyakati walizokuwa pamoja, Neymar na Mbappe walitibuana mara kadhaa wakigombea kupiga penalti. Na Mbappe alimchukiza mchezaji mwenzake, Neymar kwa kugoma kumpasia mpira. Mbappe alishinda vita yake na kuwa mfungaji wa muda wote kwenye kikosi cha PSG, alipofunga mabao 256. Neymar aliondoka PSG mwaka jana kwenda kujiunga na Al-Hilal ya Saudi Arabia, akiwa amefunga mabao 118 katika michuano yote iliyotumikia miamba hiyo ya Parc des Princes. Sasa kwenye kikosi cha Los Blancos kuna mastaa kibao wa Kibrazili, ikiwamo Vinicius Jr, Rodrygo, Endrick na Eder Militao. Mwandishi Cyril Hanouna, mwenye wafuasi 5.9 milioni kwenye mtandao wa X, alikiambia kituo cha redio cha Ufaransa cha Europe 1:

“Wabrazili wa Real Madrid ni marafiki wa Neymar. Na siku zote kumekuwa na vita kali ya Neymar na Mbappe. Neymar aliwatumia ujumbe wa kuhusu Mbappe kwa Wabrazili wa Madrid, akiwaambia wapo kwenye janga kubwa.”

Chanzo: Mwanaspoti