Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sijakata tamaa- Kaze

913646bccea6f6972301e996a1756f9e Sijakata tamaa- Kaze

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIPIGO cha mabao 2-1, dhidi ya Coastal Union ya Tanga, hakijamkatisha tamaa kocha wa Yanga Cedric Kaze ambaye amesema wameyaweka matokeo hayo pembeni na sasa wanaangalia mbele mechi zijazo.

Yanga ambao ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kesho watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kucheza na Polisi Tanzania mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa wa ushindani wa aina yake.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kaze alikiri ubora wa wapinzani wao ndio sababu ya kupoteza mchezo huo.

“Coastal walistaili ushindi, walicheza kwa bidii na kutimiza ipasavyo majukumu yao tofauti na sisi ambao nadhani tulikuwa na siku mbaya lakini ndio mpira unavyokuwa nakubali matokeo tuna mechi nyingine Jumapili (kesho) tunakwenda kujipanga kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Kaze.

Kaze alisema wachezaji wake hasa wa eneo la ushambuliaji walishindwa kutimiza ipasavyo majukumu aliyowapa na hiyo iliwapa nafasi wapinzani wao kuwatala mchezo na kupata matokeo hayo ambayo yamekuwa na faida kubwa kwao.

Alisema kitendo cha mchezaji wake Tuisila Kisinda kukosa mkwaju wa penalti na bao la mapema la Coastal Union lilionekana kuwachanganya ingawa baadaye walirudi mchezoni na kusawazisha bao lakini kitendo cha kushindwa kuzitumia nafasi walizozitengeneza nako kulizidi kuwapa ari wapinzani wao.

Kwaupande wake Juma Mgunda ambaye ni kocha mkuu wa Coastal Union, aliwapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo aliyowapa jambo ambalo lilifanikisha ushindi huo ambao umewapatia pointi zote tatu.

Alisema pamoja na matokeo hayo lakini Yanga ni timu nzuri na ngumu na aliwaambia wachezaji wake kuiheshimu kutokana na ubora wa wachezaji waliokuwa nao na anafurahi kuona lengo lao limetimia.

Mgunda alisema wataendelea kuutumia vizuri uwanja wa Mkwakwani kupata matokeo mazuri ili kujiweka kwenye nafasi nzuri sababu msimu huu wametumia muda mwingi kuimarisha kikosi chake baada ya nyota wengi kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Ushindi dhidi ya Yanga umeipandisha Coastal Union hadi nafasi ya 10, kwenye msimamo kwa kufikisha pointi 26 katika michezo 22 waliyocheza mpaka sasa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz