Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sifa 5 kocha mpya Simba, 100 waomba kazi

Simba ,kocha Mpya Simba SC

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Mpaka juzi mchana, Simba ilikuwa ina orodha ya zaidi ya Makocha 100 na bado wanazidi kutiririka tu. Lakini Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ametaja sifa tano za kocha wao mpya.

Miongoni mwa makocha ambao wametuma maombi ya kuinoa Simba wapo, Milovan Cirkovic na Zdravko Logarusic ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kukinoa kikosi hicho wengine, Josef Zinnbauer na Rulani Makwena.

Amesema kigezo cha kwanza wanamtafuta kocha mwenye ufundi mwingi katika ufundishaji wake kama ikitokea wamekutana na wapinzani ambao wazuri katika mbinu fulani aweze kubadilika kwa haraka ili kupata matokeo mazuri bila presha.

“Kigezo cha pili tunamtafuta kocha mwenye mafanikio makubwa na yanayoonekana katika soka la Afrika awe ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwani hilo ni lengo letu la muda mrefu,” amesema Try Again ambaye moja ya malengo yao kwa sasa ni kutinga hatua ya makundi ya Shirikisho kwa kuwatoa Red Arrow ya Zambia.

“Kigezo cha tatu tunamtafuta kocha mwenye uwezo wa kufundisha soka la chini na kumiliki mpira kwani hiyo ni falsafa ya Simba tangu miaka mingi katika uchezaji wake hatuwezi kubadilika.

“Tunamtafuta kocha mwenye mafanikio yake binafsi kwa maana katika timu alizopita kufundisha awali awe amechukua kutokana na kufanya vizuri pamoja na yale ya kitimu ndani au nje ya Afrika,”ameongeza na kusisitiza kuwa hawatafanya makosa kwenye uamuzi wao wa mwisho.

Amesema wanamtafuta kocha ambaye ataongeza uwezo katika kikosi cha Simba kuwa bora zaidi ya wakati huu kwani hiyo inaweza kuwa chachu ya mafanikio.

Amesema unaendelea chini ya jopo maalum ili kupata mtu makini mwenye uwezo wa kuipa Simba mafanikio katika mashindano ya ndani kwa maana ya kutetea ubingwa wa ligi, kombe la Shirikisho (ASFC) pamoja na kombe la Shirikisho Afrika.

“Sifa nyingine pia tunamtaka kocha atakayeleta ushindani wa kitimu wachezaji kushindana wenyewe kwa wenyewe na mwenye uwezo kupata nafasi ya kucheza jambo ambalo litakuwa silaha ya kufanya vizuri kwetu katika kila mechi,” amesema Try Again.

Chanzo: Mwanaspoti