Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sibomana: Tulieni, mtafurahi na roho zenu

73528 Sibomana+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA imeanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kwa kipigo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, na kuwafanya mashabiki wao kupata shida huko mitaani mbele ya watani zao wa jadi, Simba.

Si unajua mashabiki wa Yanga waliwatesa sana Simba baada ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tena ikishinda ugenini dhidi ya Township Rollers ya Botswana huku Simba ikilazimisha sare Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya UD Songo.

Sasa buana juzi Jumatano wakaenda uwanjani kuwapa mzuka vijana wao Wakimataifa, lakini dakika 90 zilipomalizika wakatoka uwanjani wakiwa wanyonge baada ya kupigwa bao 1-0 tena la mapemaaa.

Hata hivyo, winga wao mpya na kipenzi cha mashabiki wa Jangwani kwa sasa, Patrick Sibomana amezisikia kejeli za mashabiki wa Simba na fasta akawatuliza Yanga akiwaambia watulie kwani watafurahi hadi watachoka.

Sibomana akizingumza na Mwanaspoti jana Alhamisi, amesema kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi kumewaumiza na ni sawa na msiba, lakini akafichua mambo yatakaa sawa na mashabiki wataanza kushangilia mabao ya kutosha kwenye mechi zinazofuata.

Alisema kwa jinsi walivyojipanga hawakutarajia kuanza ligi kwa kipigo, lakini jambo la kufurahisha ni kuwa timu imeanza kucheza kwa maelewano na kutengeneza nafasi nyingi za mabao na tatizo lililobaki na kupasia nyavuni tu.

Pia Soma

Advertisement   ?
“Mashabiki wameumizwa na matokeo kama ilivyo kwetu wachezaji, lakini hilo si jambo la kuwaza sana. Timu inacheza vizuri na tumetengeneza nafasi nyingi za mabao japo hatukuwa na bahati,” alisema Sibomana ambaye penalti yake iliipa Yanga sare ya nyumbani dhidi ya Rollers.

Alisema licha ya matokeo hayo kuwa mabaya na yanayoumiza, lakini kwa sasa wanajipanga upya kwa ajili ya mechi zijazo na mambo yatabadilika haraka.

Hata hivyo, Sibomana alisema upya wa kikosi chao ambacho kina wachezaji wengi wapya, umekuwa ukichangia kuchelewa kupata matokeo mazuri japo wanazoeana kwa haraka.

“Tumekuwa tukicheza tofauti, inahitaji muda kidogo kuzoeana baada ya muda tutaanza kushinda vizuri, tunajua tumekosea wapi.

“Yanga tuna timu nzuri, lakini inaundwa na wachezaji wengi wapya hivyo taratibu tutakuwa sawa mashabiki watulie muda wa kufurahi ni mrefu zaidi,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz