Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shoo na heshima!

Ayoub Lakred Simba Ds.jpeg Shoo na heshima!

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo ni siku muhimu kwa Simba kuendelea kutimiza ule utaratibu wake wa kufuzu kuingia makundi ya michuano ya kwa mara 5 ikiwa tu itawafunga Power Dynamos ambayo imeufanya mchezo wa leo kuamuliwa ndani ya dakika 90 za mchezo huu wa pili hii inakuja baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2, Zambia kwenye mchezo wa kwanza.

Hakuna shaka kuwa macho yetu yapo kwa kocha mkuu wa Simba kujua atakuja na nini ili kuizima Power Dynamos ambao nao watakuwa na mpango kazi wao kuhakikisha nao wanashinda hapa ugenini.

HUYU ROBERTINHO

Ndani ya kichwa cha Roberto Oliviera kocha mkuu wa Simba kuna maeneo mengi anaonekana atayatumia kuelekea mchezo wa leo ili kumaliza mchezo na kutinga hatua hiyo ya makundi .

DAKIKA 15 ZA MWANZO

Ni kama ameingia kwenye ule muendelezo wa kupata ushindi wa magoli mengi mapema ili kuumaliza mchezo , amefanya hivyo toka msimu uliopita akiwafunga Yanga ndani ya dakika 20 hivi za mwanzo goli 2 , aliwafunga Mtibwa Manungu goli 2 za mapema kupitia kwa Jean Baleke , akaja kuwafunga Coastal na Polisi Tanzania magoli ya mapema na msimu huu ameanza kuzifunga timu nyingi goli za mapema Mtibwa tena wakiwa Manungu walifungwa goli 2 za haraka haraka , ikaja kwa Coastal Union pale Uhuru ndani ya dakika 30 walishafunga goli 3 , hii ndio silaha nadhani ataitumia tena leo.

NDANI YA MFUMO 4 : 2 : 3 : 1

Anahakikisha wachezaji wake watatu kama ilivyokuwa Zambia Kibu Dennis, Chama na Onana wanakuwa kila mara wanaongezeka ndani ya eneo la Power Dynamos na kuwafanya washambuliaji kuwa 4 hii inakuwa hatari kwa wapinzani kwani wanalazimishwa kufanya makosa .

3 : 5 : 1 : 1 ataendelea kuwapa msukumo mkubwa Power Dynamos kwa kuwafanya walinzi wa pembeni Shomari Kapombe , Mohamed Hussein kusogea juu huku viungo Mzamiru Yassin , Chama wakisogea juu zaidi na kuwaacha walinzi watatu wawili wa kati Che Malone na Kennedy Juma huku Kanoute akibaki katikati yao kwa chini akilinda shambulizi lolote la pembeni au kati kati.

4 : 3 : 2 : 1 Robertinho anatumiacwachezaji wake kurudi kwa haraka golini kwao kuzuia kwa namba kubwa lakini wakiwa na uhakika wa kumuacha mchezaji mmoja , hapo kwenye 1 : 1 wa juu ndipo alipotumia Chama na Jean Baleke kufanya mashambulizi ya kushtukiza na utulivu ukipatikana ni rahisi Simba kufunga goli nyingi tu za kutosha.

KAZI IPO HAPA!

KIBU v SOKO

Bila shaka ulikuwa mchuano bora kiasi maana mwanzoni mwa mchezo mlinzi John Soko wa Power Dynamos alianza kwa kujiamini na kupanda kila mara , hata hivyo ikawa kazi kidogo baada ya Kibu kuanza kutumia nguvu za mikimbio kwenye eneo hilo na kumfanya Soko kutopanda tena .

MULENGA Vs ONANA

Haukuwa mpambano mgumu sana kwa mlinzi huyu wa kulia wa Power Dynamos dhidi ya Willy Essomba Onana ambaye alianza kwa kasi ndani ya dakika chache za mwanzo lakini akapunguza kasi taratibu huku mlinzi Mohamed Hussein akiwa naye hapandi sana kushambulia hivyo kumfanya mlinzi huyo kuwa huru zaidi.

MUTALE v KAPOMBE

Ulikuwa ni mpambano bora sana kwa wachezaji hawa wawili na muda mwingine Joshua alihama kutoka upande huo na kwenda kwa Mohamed Hussein na kuendelea kusumbua , Joshua ndiye aliyekuwa jicho la Power Dynamos na leo bila shaka anategemea kufanya makubwa kwa sababu kijana huyo ana kipaji na ufundi mguuni .

TEMBO v MZAMIRU, KANOUTE

Kama alivyofanya kula Zambia baada ya kuwakusanya wachezaji baadhi wa kati na kuingia na mpira hadi eneo la mwisho la ushambuliaji na kumpa pasi Joshua Mutale aliyepiga krosi na kupatikana kwa goli la kwanza , inaweza kuwa ni marudio kwa mchezaji huyo kumiliki eneo la kati.

BALEKE v KATEBE, CHANDA

Baleke ataendelea kuziota nafasi alizopata dakika ya 67 , 69 , 73 na 77 ambapo alibahatika kubaki na golikipa wa Power Dynamos lakini akashindwa kumalizia na kupata ushindi bila shaka atarudi leo na sina shaka Robertinho atamuanzisha tu.

Anakutana na wachezaji wa kati wa Power Dynamos kina Katebe na Chanda walioshindwa kumkaba hasa kutokana na kuwa mipira mingi ilikuwa ikipigwa nyuma yao , sasa leo nafasi zile zikipatikana na kwa kile walichokisoma darasani wachezaji wa Simba bila shaka watawaadhibu tu .

BOYELI v MALONE

Mshambuliaji huyo wa Power Dynamos mzaliwa wa Congo hakuwa hatari na mara nyingi alicheza nje ya eneo la kushambulia kitu kilichowafanya walinzi wa Simba kuwa likizo kiasi , hata hivyo kulikuwa na makosa mawili aliyofanya Che Malone na moja la Mzamiru Yassin kupoteza pasi kwenye eneo lao la ulinzi , hii ikitokea leo inaweza kuwahukumu Simba.

CHAMA v MABEKI WA5

Chama alikuwa na siku nzuri na bora sana ndani ya Uwanja wa kumbukumbu ya Raisi Levy Mwanawasa baada ya kufunga goli zote 2 za Simba , huku akiwasumbua Lawrence Mulenga , Chiboni , Soko , Katebe na Chanda na kufunga goli mbili huku goli la pili akiwa ametembea na mpira kuwapita walinzi wa kati kabla ya kumtungua golikipa.

Hiki ndicho Chama anategemea kuendelea kukifanya hasa kutokana na kuwa na ujasiri , kipaji cha mpira , utulivu ndani ya eneo la mwisho na uwezo wa kufunga .

SIMBA NA CHAMAZI

Ni uwanja ambao klabu ya Simba imeutumia mara nyingi tu hasa kwenye michezo yake ya ligi kuu , ingawa msimu huu hawajautumia na kuna minung'uniko kuwa uwanja huo kwao ni mgumu .

Hata hivyo kiufundi uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi hauna tofauti na uwanja wa uhuru wanaotumia Simba , hivyo bado Simba wanafaida na uwanja huo kuliko Power Dynamos , Ukiuangalia uwanja unaweza kuhisi ni mdogo na hasa timu zinapoamua kurudi nyuma kuzuia huwa inakuwa rahisi na kuufanya mchezo kuwa mgumu , hata hivyo bado Simba wanafaida .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live