Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shomari: Wanasimba msihofu, tunatoboa!

Kapombe Simba G Shomari: Wanasimba msihofu, tunatoboa!

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Simba SC Shomari Kapombe amewaambia mashabiki wa klabu yake, wasiwe na wasiwasi kwani wanayo nafasi ya kufuzu hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika.

Kapombe ametoa kauli hiyo leo mchana alipokuwa anaondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kupambana na Wydad Casablanca.

"Tunazo mechi nyingi bado, tunayo nafasi ya kusahihisha makosa yetu na kufanya vizuri. Kikubwa mwalimu amefanyia kazi hasa eneo la ulinzi na ushambuliaji, nina imani tutafanya vizuri," alisema Shomari.

Simba itapepetana na Wydad Jumamosi hii Desemba 9,2023. Simba wana alama 2 kwenye makundi, Wydad hana alama yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live