Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shime afichua sababu kina Clara kutoitwa timu ya Taifa

Clara Luvanga Spain Clara Luvanga

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, Bakar Shime ametaja sababu ya kutowaita baadhi ya nyota katika kikosi kilichoingia kambini juzi kujiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake nchini Morocco zinazoanza mwezi huu ikianza na Ivory Coast.

Shime alisema kutoitwa kwa wachezaji hao akiwemo Clara Luvanga, anayekipiga Dux Logrono ya Hispania ni kutokana na kutohtajika kwa sasa.

Kocha huyo alisema; “Wachezaji wengi wana uwezo mkubwa, ila kwa sasa tumeanza na hawa kama uhitaji utakuwepo, tutawachukua michuano mingine,” alisema.

Walioitwa j ni Naijat Abas, Zulfa Mkau, Anastazia Katunzi, Happy Hezron, Christer Bahera, Vaileth Nickolaus, Zainabu Mohamed, Janeth Pangamwene, Donisia Minja Amina Ally, Stumai Abdallah, Diana Mnali, Ester Mabanza, Jamila Rajabu na Winifrida Gerald wote wakitokea JKT Queens. Wengine ni Husna Mtunda na Noela Luhala (Yanga Princess), Fatuma Issa, Koku Kipanga na Aisha Juma (Simba Queens).

Wanaocheza nje ni Julietha Singano (Juarez Singano), Diana Lucas (Amed S.F.K Uturuki), Enekia Kasongo (FC Kryvbas-Ukraine), Aisha Masaka(BK Hacken- Sweden) na Opah Clement (Beskitas- Uturuki).

Chanzo: Mwanaspoti