Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shiboub arejea kuitumikia Simba

SHIBOUB Shiboub arejea kuitumikia Simba

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKATI uongozi wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ukisema utafurahi kuona wanachukua Kombe la FA, kiungo wake wa kimataifa kutoka Sudan, Sharaf Shiboub, amerejea nchini jana.

Shiboub alikuwa amekwama nchini kwao Sudan kwa sababu ya 'lockdown' iliyosababishwa na kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona ambao ulisumbua dunia.

Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema nyota huyo amerejea nchini na ataungana na wenzake kwa ajili ya kumalizia michezo ya ligi iliyobakia na michuano ya Kombe la FA, endapo watasonga mbele.

Rweyemamu alisema ujio wa kiungo huyo, unakamilisha kikosi chao, na wanafurahi kuona nyota huyo atakuwa sehemu ya wachezaji watakaovaa medali siku watakayokabidhiwa kikombe cha ufalme wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Naye Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck aliliambia gazeti licha ya kutwaa ubingwa wa Bara, timu yake imekabiliwa na ratiba ngumu ambayo wameicheza kwa mikakati.

"Tumetoka kucheza mechi mbili hivi karibuni ambazo zilikuwa ni ngumu kwetu, licha ya kuwa tumeshafanikisha lengo la kutwaa ubingwa, bado tunahitaji kushinda mbele ya Azam FC," alisema kocha huyo kabla ya kushuka dimbani jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live