Ligi kuu ya England ipo kwénye mipango ya kutunga sheria mpya za matumizi ya fedha kwa vilabu ili kuzipunguzia nguvu za matumizi makubwa ya fedha kwa timu za Newcastle united na Manchester city zilizonunuliwa na matajiri kutoka Saudia
Hatua hiyo imefikiwa na uongozi ikishirikiana na vilabu mbalimbali baada ya uwepo wa mpango wa mabosi wa Saudia wanaomiliki Newcastle united kuwekeza katika timu mbalimbali za ulaya ikiwemo Inter milan na Bourdeúx ya Ufaransa.
Katika hatua nyingine viongozi hao wa ligi kuu wanataka kuanzia sheria hiyo ili kuwepo kwa uwiano wa matumizi ya fedha kwa timu hizo (Newcastle utd na Man city ) kulingana na vyanzo rasmi vya mapato vitakanavyo na mpira au michezo baada kufichuka kwa taarifa za uchunguzi mwaka 2018 zikiihusisha man city kumlipa mara mbili aliyewahi kuwa kocha wao Roborto Mancini nje ya chanzo mama cha mpira
Kwa mujibu wa vyanzo rasmi mmiliki wa Manchester city Sheikh Mansour amekua sehemu ya umiliki kwenye vilabu 10 katika mataifa mbalimbali ndani ya ulaya na nje.
Kwa upande wa Manchester city na Newcastle united wamekubali kuanzishwa kwa sheria hizo wakisema kuwa haziepukiki kukataliwa kwa ustawi wa mchezo huo pendwa duniani.