Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria kali kumbana OLise kule Bayern

Michael Akpovie Olise Sheria kali kumbana OLise kule Bayern

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Crystal Palace, Michael Olise ambaye yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Bayern Munich, baada ya kuzikataa timu mbalimbali kama Chelsea, atatakiwa kufuata sheria kali zilizopo katika timu hiyo ikiwa atatua.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ameripotiwa kuvutiwa na ofa ya Bayern kwa sababu anataka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Bayern tayari imeshazungumza na Palace na wanadaiwa kutoa Euro 55 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wake. Kwa mujibu wa tovuti ya Sportbible, Olise atalazimika kufuata sheria kali za Bayern kuhusu umiliki wa gari.

Bayern ina ushirikiano na kampuni ya kutengeneza magari ya Ujerumani ya Audi, ambayo inamiliki hisa za asilimia 8.33 ya timu hiyo.

Tangu mwaka wa 2002 wachezaji na wafanyakazi wa Bayern wamekuwa wakipewa magari kutoka kwa kampuni hiyo na wanaruhusiwa kuchagua aina wanayopendelea pia, huwa wanaruhusiwa kubadilisha hadi usajili.

Sheria iliyopo ni kwamba wachezaji wa Bayern lazima waendeshe kwenda mazoezini na kurudi makwao kwa kutumia magari hayo kutoka Audi, pia wanatakiwa kufanya hivyo wanapoenda katika mechi ama matukio mengine ya klabu.

Wachezaji pia wanaruhusiwa kuendesha gari aina ya Bugatti, Bentley na Porsche ambazo ni sehemu ya kampuni hiyo.

Ikiwa mchezaji atavunja sheria hiyo basi atapigwa faini na hilo limewahi kuwakuta Philippe Coutinho, Jerome Boateng, Kingsley Coman na Niklas Sule.

Mnamo Machi 2021, Coman alipigwa faini ya pauni 43,500 baada ya kwenda mazoezini akiwa na gari lake kutoka kampuni ya Mercedes.

Winga huyo alikataliwa kuingia katika uwanja wa mazoezi wa Bayern na kulazimika kuegesha gari lake barabarani.

Olise ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10 na kutoa asisti sita katika mechi 19 za Ligi Kuu ya England, atakuwa anakunja mshahara wa Pauni 220,000 kwa wiki ikiwa atatua kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Vincent Kompany.

Chanzo: Mwanaspoti