Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria Ngowi: Nimeshamaliza jezi za miaka mitano ijayo

Yanga Jezi Mdg Sheria Ngowi: Nimeshamaliza jezi za miaka mitano ijayo

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunifu maarufu wa mavazi nchini ambaye amekuwa akibuni jezi za Klabu ya Yanga, Sheria Ngowi amesema kuwa tayari ameshamaliza kubuni na kuandaa jezi za misimu mitano ijayo.

Kauli hiyo ya Ngowi ameitoa wakati akihojiwa na Clouds FM ikiwa ni saa chache baada ya Yanga kuachia uzi mpya kwa ajili ya michuano ya Kimataifa ya CAFCL itakayoanza kesho huku akisema kuwa anasubiri uongozi wa Yanga upitishe tu.

“Sifikirii kufanya kazi na klabu nyingine, nimeamua hilo kwa sababu naheshimu riziki Yangu ndani ya Yanga.

“Tayari jezi za misimu mitano mbele za Yanga nimeshamaliza kuzibuni na ninachosubiri kwa sasa ni ruhusa Kwa viongozi nizitoe muda ukiwadia,” amesema Ngowi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: