Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sherehe ya kumfunga Simba, mashabiki wa Yanga waitwa kunywa supu Jangwani

Kamwe  Instagram Sherehe ya kumfunga Simba, mashabiki wa Yanga waitwa kunywa supu Jangwani

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya yanga wameitwa kwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Klabu hiyo zilizopo Mtaa wa Twiga na Jangwani, Kariakoo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kunywa supu kusherehekea ushindi wa bao 5-1 walizomfunga mtani wao Simba SC Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkapa.

Afisa Habari Yanga SC, Ally Kamwe amesema hayo baada ya ushindi dhidi ya Coastal Union Jijini Tanga akisema mpaka sasa wameshapewa ng'ombe 10 kama zawadi hivyo mpango wao ni ni kuchinja ng'ombe hao na kunywa supu na mashabiki.

“Michezo 9, alama 24, hii imaana kwamba taa ya kijani imewaka sasa tunakwenda mdogo mdogo tunapunguza pointi. Tumemaliza mechi yetu na Coastal Union, Ligi inakwenda kusimama kwa wiki mbili.

“Sisi kama Yanga rasmi niwatangazie mashabiki na wanachama wa Yanga kwamba sherehe za goli tano ndiyo zinaanza rasmi leo, tulikuwa hatujasherehekea kabisa, tulikuwa kimya na kama mliona tuna furaha basi tulikuwa tunadokoa tu kidogo.

“Taarifa nilizo nazo mpaka sasa tuna ng’ombe 10, tumepewa kama zawadi. Tunaandaa utaratibu, Wanayanga tutakutana Jangwani (Makao Makuu ya Yanga), Jumapili asubuhi kunywa supu. Tutachinja ng’ombe, tutakunywa supu.

“Kila mwanayanga atoke nyumbani na maandazi, chapati, vitumbua, mikate, supu ataikuta Jangwani. Wanayanga wajiandae tunakwenda kunywa supu Jumapili,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: