Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shemeji wa Mayele ashangazwa na stori za majini

Mayele Jierre Shemeji wa Mayele ashangazwa na stori za majini

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: ManaraTV

Mwandishi wa Habari, Jierre Sakisa ambaye ni raia wa Congo DRC amesema anamfahamu vyema mshambuliaji wa Pyramid na Congo DRC, Fiston Mayele kwa kuwa ni shemeji yake.

Jierre ambaye ni shemeji wa Mayele yuko nchini kwa ajili ya mchezo wa Yanga SC dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaofanyika kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutua nchini Jierre ameshangazwa kukutana na taarifa za Mayele kuhusu mambo ya Majini na kusema Mayele anayemjua hana mambo hayo.

“Tunafahamiana tangu udogo wetu. Ni mchezaji mzuri sana na safari yake ya mpira ilianzia katika Mji wa Likasii kabla hajaelekea Kolwezi ambako alionekana zaidi.

“Tulimtambua haraka kutokana na uwezo wake wa kupachika magoli mengi na baada ya hapo alijiunga na klabu ya As Vita ya Kinshasa nadhani baada ya hapo kila kitu kinaonekana ni kipi alikifanya.

“Mimi na Mayele ni mtu na shemeji yake amemuoa dada yangu anayeitwa Sharlene, nimeshangaa kusikia taarifa za masuala ya Majini. Kiukweli huyu sio Mayele ninayemjua,” amesema Jierre.

Chanzo: ManaraTV