Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh Jassim kutua West Ham

Sheikh Jassim Fd Sheikh Jassim

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tajiri wa Qatar, yule aliyetaka kuinunua Manchester United, Sheikh Jassim ameripotiwa kuwa na mpango wa kununua hisa kwenye klabu ya West Ham United ili kutimiza ndoto zake za kuwa na timu Ligi Kuu England.

Sheikh Jassim anataka kuinunua West Ham United baada ya mmiliki mwenza wa kikosi hicho, mrembo Vanessa Gold kutangaza kuweka sokoni baadhi ya hisa.

Mrembo Vanessa anamiliki asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo alizorithi kutoka kwa baba yake, David aliyefariki dunia Januari mwaka huu.

Kinachoelezwa mrembo huyo amepanga kuuza asilimia 10 ya hisa zake, lakini yupo tayari kuuza zote kama atapatikana mteja sahihi.

Mpango wa Sheikh Jassim umekuja baada ya kushindwa kuinunua Man United. Vanessa ameipa benki ya Rothschild kusimamia mpango huo baada ya kujadiliana na wawekezaji wengine wa West Ham United, David Sullivan, Daniel Kretinsky na Tripp Smith.

Tajiri huyo wa Qatar anahitaji kuwa na timu kwenye Ligi Kuu England na aliwahi kuhusishwa pia na mpango wa kuinunua Tottenham Hotspur mapema mwezi huu.

Na sasa amepanga kuichukua West Ham ambayo imekuwa maarufu kwenye Jiji la London kutokana na mashabiki kujaa uwanjani kwenye kila mechi inazocheza.

Chanzo: Mwanaspoti