Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehat asaini miaka mitatu Al Ahly

Bf5cab74 2a3a 4f0b Ab52 140de155757f.jpeg Shehat asaini miaka mitatu Al Ahly

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa klabu ya Al Ahly, Hussein El Shahat raia wa Misri ameongeza mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu hiyo mkataba ambao utaisha mwaka 2026.

El Shahat mwenye umri wa miaka 31 alikuwa analipwa mshahara wa dola 83,000 (zaidi ya Milioni 190 za Kitanzania) kwa mwezi

Baada ya kuongeza mkataba mpya kwa sasa atakuwa analipwa mshahara wa dola 100,000 (zaidi ya milioni 230 za Kitanzania) kwa mwezi na kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa Al Ahly sawa na Percy Tau raia wa Afrika Kusini na Ali Maaloul raia wa Tunisia wanaolipwa mshahara huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live