Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheffield kumtimua Kocha leo

Skysports Sheff Utd Boss Paul Heckingbottom 6379950 Paul Heckingbottom

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sheffield United inatarajia kumfukuza kazi Paul Heckingbottom leo hii na kumgeukia meneja wa zamani Chris Wilder katika jaribio la kufufua kampeni yao ya Premier League

Sheffield United wako mkiani mwa jedwali wakiwa wameshinda mara moja pekee msimu huu na kulala kwa aibu ya 5-0 dhidi ya Burnley wikendi. The Blades pia wameruhusu mabao 39 kwenye ligi katika michezo 14 ya ligi.

Kuondoka kwa Heckingbottom huko Bramall Lane inamfanya kuwa meneja wa kwanza kufukuzwa kazi kwenye Premier League msimu huu.

Kufikia hatua hii mwaka jana, mameneja watano walikuwa wameondolewa kwenye nyadhifa zao: Scott Parker (Bournemouth), Thomas Tuchel (Chelsea), Bruno Lage (Wolves), Steven Gerrard (Aston Villa) na Ralph Hasenhüttl (Southampton).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live