Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaw, Bissaka bado sana Man United

Aron Wan Bissaka Shaw, Bissaka bado sana Man United

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabeki wa klabu ya Manchester United Luke Shaw na Aaron Wan Bissaka wanatarajiwa kuendelea kukaa nje ya uwanja kwa muda zaidi baada ya kupata majeraha.

Luke Shaw ambaye aliumia kabla ya Wan Bissaka anatarajiwa kurudia uwanjani mwezi Novemba baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, Huku ikikadiriwa na Wan Bissaka nae atakaa nje ya uwnaja kwa kipindi hichohicho.

Mabeki hao ndio wamekua mabeki chaguo la kwanza ndani ya Manchester United kwa upande wa kulia na kushoto, Hivo ni wazi kukosekana kwao kutaendelea kuigharimu timu hiyo katika michezo ijayo.

Beki Luke Shaw amekua kwenye kiwango bora sana chini ya kocha Erik Ten Hag jambo ambalo limemfanya aendelee kua chaguo la kwanza ndani ya timu hiyo lakini bahati mbaya ni kwasasa hataweza kuwepo uwanjani kuitumikia timu hiyo.

Wan Bissaka ambaye alikua akikaribia kutolewa kwa mkopo katika dirisha dogo lililopita mwezi Jnauari, Lakini alipambania nafasi ndani ya timu hiyo mpaka kua chaguo la kwanza la mwalimu ni wazi kukosekana kwake kwasasa ni pengo ndani ya Man United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live