Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaqiri awanyamazisha waliotoa kejeli

Shaqiri Xerdan Xherdan Shaqiri

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Uswizi, Xherdan Shaqiri, amethibitisha kuwa adui wa Serbia kwa mara nyingine kwa kuwasaidia vijana wa Dragan Stojkovic kwenda 16 bora michuano ya Kombe la Dunia hapo jana kwenye Uwanja wa 974.

Shaqiri alifunga bao la ushindi dakika za mwisho dhidi ya Serbia katika mashindano ya mwaka 2018 nchini Urusi na kusherehekea kwa kutengeneza umbo la tai kwa mikono yake kuonyesha kuunga mkono Kosovo, nchi alikozaliwa na jimbo la zamani la Serbia lililojitangazia uhuru mwaka 2008, Uhuru ambao Serbia wamegoma kuutambua.

Mchezaji huyo wa Chicago Fire, alizomewa na kukejeliwa wakati shabiki mmoja wa Serbia alitolewa nje kwa kuimba nyimbo za kejeli.

Shaqiri na Taifa lake la Uswizi watacheza hatua ya 16 bora siku ya Jumanne dhidi ya Ureno huku kila mmoja akiuhitaji ushindi huo ambao utafanya aende hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live