Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaktar Donetsk yahofia kumpoteza Novatus Dismas

Novatus Dismas 40 Shaktar Donetsk yahofia kumpoteza Novatus Dismas

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni miezi miwili sasa tangu Shaktar Donetsk ya Ukraine kufanya mabadiliko kwenye benchi lao la ufundi kwa kumfukuza mwalimu Patrick Van Leeuwen na mikoba yake kupewa Marino Pusic (52) kukinoa kikosi hicho mpaka mwaka 2025-2026.

Tangu kufanyika kwa mabadiliko ya benchi la ufundi kijana wa Kitanzania ambaye alifanya vizuri sana kwenye michezo kadhaa aliyopewa nafasi ya kucheza, hapa namzungumzia Novatus Miroshi Dismas ambaye kwa sasa hana tena nafasi katika kikosi hicho na muda mwingi anakalia ubao.

Hata hivyo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwanini Novatus anakaa sana benchi, Je hana uwezo? au mabadiliko ya benchi la ufundi ni sababu ya kijana huyu kutopata nafasi?

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari Nchini Ukraine amenukuliwa akisema kwamba “Sitaki kuamini kama sababu ni uwezo wake lakini kitendo cha Novatus kwenda hapo kwa mkopo akitokea Zulte naamini kuna hofu ya Shaktar kuendelea kumtumia kwakuwa wanahofia kumuweka kwenye njia ya kununuliwa na timu nyingine, kitu ambacho wao Shaktar hawanufaiki na chochote”

Kisha akamalizia kwa kusema “Ulaya vinaenda tofauti sana watu wanaangalia pesa kwanza”

Kitu cha msingi hapa ni kuelewa kwamba Shaktar Donetsk ni miongoni mwa vilabu vinavyouza wachezaji kwenye timu nyingi Ulaya, ukiachana na klabu kama Ajax, Brighton, Tottenham, Sporting Lisbon, Dortmund nk.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live