Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shakira: Nilisimama kufanya muziki sababu ya Pique

Shakira And Gerard Pique Shakira: Nilisimama kufanya muziki sababu ya Pique

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa mwimbaji Shakira amekiri kuwa alisitisha kazi yake ya muziki wakati akiwa kwenye uhusiano na mume wake wa zamani, mwanasoka Gerard Pique. Akipiga stori na Jarida la The Times, Shakira amefunguka kuwa;

"Kwa muda mrefu nilisimamisha kazi yangu, kuwa karibu na Gerard, ili aweze kucheza soka, nilifanya yote hayo kwa upendo"

Mwimbaji huyo wa wimbo maarufu wa 'Hips Don't Lie' ameongeza kuwa kutengana na Pique ilikuwa kipindi kigumu sana kwake;

"Kilikuwa kipindi cha giza zaidi maishani mwangu, niliwaza watoto wataishi vipi, isitoshe tulikuwa tumeishi pamoja kwa muda mrefu mno” - Shakira.

Wawili hao walitengena mnamo mwaka 2022 baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 12 na wana watoto wawili wa kiume. Baada ya kutengena, Gerard aliingia kwenye uhusiano na mpenzi wake mpya Clara Chia, mwenye umri wa miaka 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live