Klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine anayechezea nyota wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ukraine kwa mara ya 15 kihistoria kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Dynamo Kyiv.
Klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine anayechezea nyota wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ukraine kwa mara ya 15 kihistoria kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Dynamo Kyiv. Shakhtar Donetsk imetwaa ubingwa huo ikiwa na pointi 70 baada ya mechi 28 wakiwa pointi 7 mbele ya Dynamo Kyiv iliyopo nafasi ya pili pointi 63 baada ya mechi 28 huku zikiwa zimesalia mechi mbili pazia la Ligi hiyo kufungwa.