Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda awachana Simba "Kuna vitu havipo sawa"

Dauda Shaffih Ml Shaffih Dauda

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka, Shaffih Dauda amedai kuwa kuna tatizo ndani ya Klabu ya Simba hali inayopelekea mambo yao kutokwenda sawa na kupishana baadhi ya mambo.

Kauli hiyo ya Dauda inakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Simba kuachana na mshambuliaji wao, Dejan Georgijevic raia wa Serbia.

"Mimi niliwaambia kuwa kuna vitu havipo sawa ndani ya Simba, ni juzi tu nilitoka kuwaambia hapa hapa mkaona nawakebehi, mkahisi siwatakii mema na kuamini nina agenda binafsi.

"DIGALA sipo hapa kuonea mtu wala timu, sipo hapa kusema uongo ili kiwe nini? Huko tushapita, kila nikitaka niwape dawa naona mnakimbia drip kwa kuamini panadol inatosha kupooza maumivu.

"Jana pia nimetoka kuwaambia mkishaenea darasani mwambieni Kiranja aje kuniita niwape darasa zuri sana Simba ila mkakaidi, kwasasa nawapa muda mjitafakari kisha DIGALA nitazungumza kuwaambia wapi mnakosea huko ndani.

"Kubalini drip la DIGALA liwaingie, ni dawa nzuri sana kuliko hizo panadol zenu mnazopeana kuwa nawachukia, nawapenda sana, nataka niwaweke sawa.

"Nasubiri Press Release nipo pale nimekaa, mkienea darasani basi mtumeni Kiranja aje kuniita. THIS IS DIGALA."
ameandika Shaffih kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live