Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda aishukia Simba

Barbara Gonzales CEO Simba Barbara, CEO wa Simba

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna dunia ambayo Simba wanaishi, ni dunia ambayo wanaamini hakuna makosa, wanaamini ni wakubwa, wanaamini kila kitu kinachofanyika ni sahihi sana.

Hata pale ambapo wameharibu watahitaji kupamba na kuonekana hawajaharibu, hata pale watapopaswa kuambiwa maneno machungu ya ukweli watahitaji nyimbo za mapambio.

Siku chache zimesalia kuelekea Ngao ya Jamii hawana jezi mpya, masaa yamesalia kuelekea Simba Day hawana jezi mpya, lakini ndio klabu hii ambayo tunalazimishana kuiita kubwa, klabu yenye weledi? Excuse me.

CEO kama Mtendaji wa klabu you are in for this, suala la jezi sio option ni lazima, suala la merchandise ni compulsory na linafahamika, inatia ukakasi kwa namna mnavyoyaendea mambo, inafikirisha sana.

DIGALA siwezi kukubali kuwa kwenye dunia ya praise and worship, sio dunia nzuri ya kuficha makosa na kuonekana mema, sio dunia nzuri mambo yakienda mrama watu wasake namna ya kujificha sio sawa na hii ni AIBU.

Kwa Shabiki wa Simba anayejua mpira na kuelewa maana ya biashara anafahamu kuwa hili mmeharibu, lakini kwa Shabiki yule oya oya tu ataona DIGALA nachonga, ataona Digala ana nongwa ila in details nawapa dawa ya kuwaponya.

Kwakuwa hili mmeshaharibu sio vyema msimu wa 2023/24 mkarudia tena makosa, hakuna excuse kwa matukio ambayo yana time frame, hakuna excuse ya Mdhamini wala usafiri, jezi sio suala la bahati mbaya.

Hakuna wimbo wa maana utakaotungwa kuepusha aibu hii, hakuna wimbo utatungwa kuepusha kadhia hii, ndio ni klabu maarufu sasa pambaneni kuusaka UKUBWA, ukubwa una details zake, ukubwa una indicators zake, BADILIKENI.

DIGALA naamini mpira ni darasa kubwa, utawala ni darasa kubwa, muda wa kuendelea kujifunza upo na naamini tukae darasani kama Wanafunzi watiifu na sio Walimu wakorofi.

DIGALA

Chanzo: www.tanzaniaweb.live