Klabu ya Yanga jana Agosti 3 ilitangaza kuzindua Doccumentaru yake ya matukio yote ya msimu wa 2022/23 ya Klabu ya Yanga.
Sasa Mchambuzi na mdau wa Soka Shaffih Dauda amekuja na wazo ambalo anaona Yanga wanaweza kupiga hela kama wataitumia vibaya platform hiyo. Akizungumza Shaffih amesema;
"Yanga leo wametangaza ujio wa documentary yao nimeona watu wakitoa maoni kila mmoja kwa utashi wake lakini tafsiri yake ni nini ? Kizazi kilichoshuhudia historia fulani kinaweza kuona jambo ni la kawaida lakini nawaelewa Viongozi matukio kama haya kuna wakati hayahitaji simulizi za maneno hasa kizazi hiki ya kushare link ."
"Viongozi wataondoka , Wachezaji wameanza kuondoka kumbukumbu ya clip pekee haitoshi , wazo la kuunganisha matukio ya Msimu mzima na kuyaweka kwenye package moja ni unoma 100%."
"Sina shaka na viongozi vijana pale Jangwani lakini nimewaza nje ya box kidogo , hili inawezekana lipo kwenye mipango yao lakini kama halipo sio mbaya wakaliongeza na hili , Hii Documentary isiishie tu juu juu ! Siku hizi Dunia imehamia Netflix na vijana wote wajanja wapo huko waone namna wanaweza kufanya sisi wadau wa Netflix tulipie tuishi nayo ."
"All in all congratulations kwa team kuja na wazo hili supa.