Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Simba SC wanamtamani Maxi Nzengeli

Shaffih Max Nzengeli Shaffih Dauda: Simba SC wanamtamani Maxi Nzengeli

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati ndio kwanza akiwa ameanza kuuwasha moto ndani ya Kikosi cha Yanga, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Maxi Mpia Nzengeli ameshakuwa gumzo kwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini.

Hilo linathibitishwa na Mchambuzi nguli wa Michezo Shaffih Dauda ambae anasema kwa uwezo wa Maxi mpaka Mashabiki wa Simba SC wanamkubali Mcongo huyo.

Akizungumza Shaffih anasema;

"Mimi nimefarijika sana kuna mashabiki wa Simba wale kindakindaki wamekaa wanamsifu Max Nzengeli ,wanasema kabisa huyu ni mchezaji sio huyo tu wapo mashabiki wa Simba wamekaa wanasema kabisa Yanga wana timu"

Je, ni kweli Maxi anakubalika kwa kiasi hiko kwa Mashabiki wa Simba SC? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live