Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Kama Simba wanamtaka Kibu, wasikilize anachokitaka

Kibu Kuwasili.jpeg Kibu Denis

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimeona na kusikia mjadala unaomuhusu Kibu Denis kuhusu thamani yake ya sasa ambapo mkataba wake na Simba umebakiza siku chache kumalizika.

Watu wengi wanasema Kibu hana thamani ya Tsh. 600 milioni ambayo ndio inatajwa, kitu kikubwa na muhimu tunachotakiwa kujua/kufahamu thamani ya mchezaji inatokana na nini?

Thamani ya kwanza ya mchezaji inatokana na thamani ya mkataba alionao na timu yake ya wakati huo. Kwakuwa mkataba wa mchezaji unaelekea mwisho, maana yake anakuwa mchezaji huru.

Mchezaji anapokuwa huru ‘free agent’ maana yake anapojiunga na klabu nyingine hakuna transfer fee inayolipwa, ndio maana wachezaji wengi wakitaka kuondoka kwenye timu wanasubiri hadi mkataba uishe kabisa ili akapige hela nyingi kwenye timu itakayomsajili kwa sababu kuna kuwa hakuna gharama za uhamisho.

Kitendo cha Simba kushindwa kumuongeza Kibu mkataba mapema kabla haujakaribia mwisho ndio kimepelekea haya yote tunayoyaona leo.

Kama kuna timu ingekuwa inataka kumnunua Kibu akiwa bado ana mkataba na Simba maana yake kuna ada ya uhamisho ingelipwa, kama Simba ingemuuza ingehitaji kiasi gani? Ingemuuza chini ya Tsh. 400 au 300 milioni?

Kwa hiyo kama Simba ingemuuza Kibu kwa Tsh. 300 milioni, na yeye ameongezea hapo mishahara yake ya miaka mwili ndio inakuja ileile Tsh. 600 milioni au zaidi ya hapo.

Kama Simba wangemwita Kibu mezani mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kuisha wakae wajadili kuhusu mkataba mpya, thamani yake isingeweza kufikia hii ambayo inatajwa sasa.

Kwa sababu Simba walishindwa kufanya mazungumzo mapema ya kuongeza mkataba wa Kibu kwa sababu wanazozijua wao, kwa hiyo kwa sasa Kibu ndio mwenye nguvu ya kuwaambia Simba chochote anachotaka!

Na ukiangalia Kibu ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo, kwa hiyo kwa kipindi hiki Simba hawana nguvu kwenye makubaliano ya kumbakiza Kibu. Ndio maana mchezaji anakuja na matakwa yake na kama Simba watashindwa haimaanishi kwamba atashindwa kupata sehemu nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live