Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki wa Yanga aahidi milioni 1 kila bao "Wananchi mtakunywa supu"

Nyanzala Hussein Makubi Ng’wananyanzala.

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa Klabu ya Yanga, Hussein Makubi Ng’wananyanzala kutoka mkoani Geita ameahidi kutoa kiasi cha Tsh milioni moja kwa kila goli ambalo timu za Tanzania zitafunga kwenye mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba na Yanga watakuwa na vibarua vigumu weekend hii kusaka tiketi ya kuingia nusu fainali ya michuano hiyo ambapo Mnyama atavaana na Al Ahly wakati Wananchi wakiutafuna mfupa mgumu wa Mamelodi Sundowns.

“Ninampongeza Rais Samia Sami kwa kuwapa hamasa vijana ili waweze kupambana kwenye michezo. Siwezi kumpongeza mama kwa maneno tupu, kama kawaida kwenye goli la milioni tano la mama mimi nitaongeza Tsh laki 5.

“Kwa kuwa mama emongeza Tsh milioni 10, na mimi nitaongeza milioni 1 katika kila goli kwa mchezo wa kimataifa. Mchezo tunaoenda kucheza sasa hivi Yanga dhidi ya Mamelodi kwa kila bao nitatoa Tsh milioni 1. Hata watani zetu Simba wakifunga, nitaongeza milioni moja kwenye pesa ya hamasa ya mama kwa kila goli.

“Najua watani zangu wakisikia pesa, hawatacheza kwa mzaha, kwa hiyo watakaposhinda nipo tayari kuwapa hiyo pesa. Hata mwaka jana niliwapa milioni 3.5 kwa magoli saba, kwa hiyo na mwaka huyu naomba wapate hamasa ya juhusu.

“Lakini ninaowaombea zaidi kufanya vizuri ni Yanga kwa sababu mimi ni mwanachama wa Yanga kindakindaki. Ninaiombea Yanga ishinde bao nyingi nitatoa pesa.

“Mashabiki wa Yanga wajiandae iwapo tutamfunga Mamelodi basi watakula supu ya ng’ombe kwa sababu tutachinja ng’ombe na kula supu, tutafunga mtaa mmoja lakini hata mikoa mingine wanaweza kuiga. Hata mwanasimba atakaribishwa akija na jezi ya timu yake atapewa ugeni rasmi atapewa supu kwenye sherehe ya Yanga.

“Ninaombe mashabiki wote na Watanzania wote tujitokeze kwenye uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kushuhuduia mchezo huo na kuwapa hamasa wachezaji wetu ili wapate ushindi,” amesema Ng’wananyanzala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live