Tukio hilo lilitokea katika eneo maarufu, lililo na baa la Milan liitwalo Navigli, muda mfupi baada ya saa sita usiku Jumatatu.
Shabiki huyo wa Newcastle anaripotiwa kuwa katika hali nzuri hospitalini baada ya kuchomwa kisu mjini Milan kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa katika jiji hilo la Italia.
Vyombo vya habari vya Italia vinaripoti kwamba mwanamume mwenye umri wa miaka 58 alidungwa kisu mara tatu – mara moja mgongoni na mara mbili kwenye mkono.
Tukio hilo lilitokea katika eneo maarufu la Milan liitwalo Navigli, muda mfupi baada ya saa sita usiku (2200 GMT) siku ya Jumatatu.
Haijulikani ikiwa ilitokea wakati wa pambano kati ya mashabiki wa kandanda hasimu au lilikuwa tukio tofauti.
AC Milan watakuwa wenyeji wa Newcastle baadae Jumanne katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.