Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki azinguana polisi, apigwa mwana ukome

Utataaaaa Shabiki azinguana polisi, apigwa mwana ukome

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Video inayosambaa mtandaoni inamuonyesha ofisa wa polisi akimpiga shabiki mmoja usoni kabla ya kumuangusha na kumtuliza sakafuni.

Ripoti kutoka tovuti ya The Sun, zinaeleza kuwa shabiki huyo alikuwa amemrushia polisi huyo chupa, ingawa katika video hiyo ilionekana amemrushia kikombe cha plastiki kilichojaa bia.

Video hiyo inamuonyesha shabiki huyo akizunguka kundi kubwa la watu akiwa na bia mkononi kabla ya kumrushia askari huyo.

Shabiki huyo aliyeonekana kuwa na hasira baada ya kurusha kikombe hicho alikuwa akitembea kumsogelea askari kana kwamba anaenda kupigana naye.

Lakini kabla hajatimiza dhumuni lake baada ya kumsogelea askari alipigwa ngumi ya uso iliyomfanya ashindwe kuvumilia na kudondoka chini.

Baada ya kudondoka, askari alimkalia kwa juu na kuanza kumzuia kisha maofisa wengine waliwasili na kuanza kumsaidia mwenzao kumdhibiti shabiki huyo,

Mashabiki wengine walikuwa wamesimama tu wakitazama mzozo huo ukiendelea, na baada ya dakika kadhaa askari wa kutuliza ghasia walianza kuwaondoa.

Tukio hilo lilitokea juzi wakati Poland inamenyana na Austria huko Berlin na mchezo ulimalizika kwa Austria kushinda mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Olympic na kuiondoa Poland katika michuano.

Kipigo hicho kimeifanya Poland kuwa timu ya kwanza kutoka katika michuano hiyo licha ya kuwa na mchezo mmoja mkononi.

Mbali ya tukio hilo, pia kulikuwa na tukio lingine la shabiki wa Poland aliyedondoka jukwaani ambaye aliwahishwa hospitalini.

Chanzo: Mwanaspoti