Katika mchezo kati ya Ureno na Bosnia & Herzegovina, Jumatatu iliyopita Cristiano Ronaldo alijikuta kwenye maumivu baada ya mmoja wa mashabiki kumkanyaga mguuni ikiwa ni katika harakati za kutaka kupiga picha na staa huyo.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka The Sun ni kwamba tukio hilo lilitokea dakika 38 ambapo video ilionyesha shabiki mmoja akiruka kutoka jukwaani na kuvuka mabango ya matangazo ya pembeni mwa uwanja kisha akaingia ndani.
Baada ya kuingia akakimbia haraka na kumfikia Ronaldo ambaye muda huo alikuwa anajiandaa kurusha mpira, licha ya dhamira ya staa huyo kuwa ni kupiga picha lakini katika purukushani na haraka zake akajikuta anamkanyaga Ronaldo kwenye mguu wake wa kulia na kumuachia maumivu.
Ronaldo alionekana kuumia na akawa anachezesha mguu wake baada ya walinzi kuingia na kumtoa shabiki huyo. Katika mchezo huu Ronaldo alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 5-0 ambao Ureno iliupata.
Mastaa wakubwa wamekuwa wakikutana na kadhia ya mashabiki kutaka kupiga nao picha hata wakati ambao wana ratiba tofauti.