Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki akiyevamia uwanjani fainali ya UEAF akomba bilioni 1

Youtube Mellstroy Sd Shabiki akiyevamia uwanjani fainali ya UEAF akomba bilioni 1

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtengenezaji wa maudhui katika mtandao wa YouTube Mellstroy raia wa Urusi alitoa challenge kwa yeyote atakayekimbia uwanjani wakati wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley kati ya Real Madrid dhidi ya Dortmund huku akiwa ameandika jina la YouTuber huyo nyuma ya jezi yake atashinda £300k sawa na shilingi bilioni 1 za Kitanzania.

Dakika chache baada ya mchezo wa fainali kuanza ndani ya dimba hilo la Wembley, Mashabiki wawili waliingia uwanjani huku shabiki mmoja akiwa ameandika Jina la YouTuber Mellstory kwenye jezi yake aliyoivaa.

Kutokana na masharti ya challenge hiyo huenda jamaa aliengia akiwa ameandika Jina la YouTuber huyo akajishindia kitita Cha fedha £300k sawa na Tsh Milioni 900 za Kitanzania.

Lakini pia huenda akakutana na adhabu ya kuzuiwa kuingia kwenye viwanja vyote nchini Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live