Shabiki wa soka wa Brazil amefariki dunia siku mbili baada ya kupigwa na chupa ya bia wakati akiwa nje ya Uwanja wa Sao Paulo.
Tukio hilo lililotokea baada ya ugomvi kuzuka wakati baadhi ya mashabiki wakingojea kuingia uwanjani.
Klabu ya Palmeiras inayocheza kwenye uwanja huo imesema haikubaliani na mauaji ya kinyama ya Gabriella Aneli (23)kwenye eneo ambalo ni la burudani.
Gabriela alipatwa na mashambulio mawili ya moyo, alikimbizwa hospitali, akafanyiwa upasuaji lakini juhudi zote za kuyaokoa maisha yake zilifeli.
Klabu hiyo imesema kuwa kitendo hicho kinatia doa kwenye soka la Brazil na imetaka polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.