Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Yanga aipa Simba mbinu kuiua Kaizer

Kaizer Pic Data Shabiki Yanga aipa Simba mbinu kuiua Kaizer

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SIMBA ni mwenyeji wa Kaizer Chiefs mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam baada ya awali kupoteza kwa mabao 4-0.

Mwanayanga kindakindaki Jerry Wasley ameaiambia Mwanaspoti kuwa, Simba ili aweze kupata matokeo katika mchezo huo anatakiwa kuwaheshimu wapinzani wake.

Amesema, katika mchezo huo atashinda Simba lakini kumtoa Kaizer katika nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali itakuwa ngumu kutoka na idadi ya mabao ambayo watatakiwa kuyapata katika mchezo huo.

"Simba akicheza kwa nidhamu anaweza kushinda mchezo huo lakini hawezi kuwatoa Kaizer," amesema Jerry na kuongeza kuwa tayari ameishanunua jezi yake tayari kutua kwa Mkapa kesho kuwasapoti Kaizer.

Aidha Jerry amesema amesema kaishajifunza na namna gani ya kuongea na mashabiki wenzake kutoka Afrika Kusini akijinadi na kusema; "Hlonipha Inkosi ikiwa na maana kwamba show respect to chief," amesema Jerry.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz