Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki: Tano zunauma nyie acheni tu

Aziz Skudu Insta Shabiki: Tano zunauma nyie acheni tu

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Napingana na wanasimba wenzangu wote wanaosema kufungwa goli tano ni Jambo la kawaida.

Hapana, historia inaonyesha Simba au Yanga mara zote kufungwa goli nyingi kunakuwaga na sababu kubwa ya Usaliti au Migogoro ndani ya hizi timu.

Rejea ushindi wetu wa 5-0 kwa Yanga,walikuwa ktk Mgogoro mkubwa sana. Simba kwa mara ya kwanza tumefungwa na mtani wetu bila ya uwepo wa Mgogoro wowote ndani ya timu.

Tumezidiwa mbinu,Uwezo na Ubora wa Mchezaji mmoja mmoja. Tukiwa serious hiki kipigo tunaweza kukitumia kama darasa dhidi ya usajili wa makocha,Wachezaji na Uendeshaji wa timu wa kisasa.

Hakuna timu serious inaweza kumtoa Mchezaji kutoka majeruhi kuja uwanjani katika mechi kubwa tena bila sababu ya msingi ya kuacha wachezaji wenye ubora kwa wakati huo.

Simba imefungwa ikiwa watu wote muhimu ni sehemu ya uongozi wa timu. Ukweli,Uwazi,uwajibikaji,weredi na upendo kwa timu ndiyo hitaji la simba kwa sasa. Sikuwahi kujua mpira unamaumivu sawa na Msiba mzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live