Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba achafukwa; Ningekuwa karibu ningemzaba vibao Ahmed Ally

Ahmed Ally LEO Ahmed Ally.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome ameonesha kukerwa na kitendo cha Meneja Habari wa Klabu hiyo, Ahmed Ally kutokana na kauli zake za kuwatukana watani zao Yanga.

Mchome amesema hayo baada ya Ahmed kudai kuwa klabu zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Afrika akiwalenga Yanga kuwa ni 'washamba' hivyo hawana la kujifunza kutoka kwao kwani wao wameingia hatua hiyo mara nne.

“Anayeumia kwa Yanga kufuzu robo fainali ana sababu zake binafsi. Nimefuatilia press ya msemaji wetu Ahmed Ally, anasema ‘wamefuzu washamba washamba’, ile kauli imeniboa sana, sio kauli nzuri kwenye soka.

“Huyu msemaji mimi naona kama anatuzingua Wanasimba, tumtafakari kwa umakini, yale ni matusi. Yanga ametufunga sisi bao 5, hakuna sehemu ambapo alikwenda akatutukana. Ahmed kama hana fact za kuzungumza mbele za watu aache, yanamuangusha.

“Alianza kusema mafanikio ya Yanga wa kushukuriwa ni Mo Dewji, watu wanajiuliza huyu msemaji akienda kwenye press zake huwa amepasha ama? Inawezekana wanamminyia cha kupima. Anasema waliofuzu ni washamba kwa hiyo Mamelodi ni washamba? Petro De Luanda, Esperance, Al Ahly ni washamba?

“Unaposema ukifuzu unamfuata mkubwa mwenzako maana yake unamfuata Yanga ambaye tayari ameshafuzu. Ndio maana Mzaramo alisema mashabiki wa Simba ni 'madunduka…' leo tunagombani nafasi ya pili na Jwaneng Galaxy.

“Unaziita timu ni washamba, wewe Simba unao uwezo wa kumfunga Mamelodi? Leo waseme nusu fainali ni Simba na Yanga, wewe utaweza kumfunga Yanga au utasimamisha minara mingine Kwa Mkapa.

“Unapomtukana mtu ambaye hauchezi naye, haupo naye kundi moja, huo ni wivu wa maendeleo, ni roho mbaya na uchawi na unatugombanisha sisi mashabiki wa Simba na wa Yanga. Sisi tunachohitaji ni mafanikio ya Klabu.

“Tuache kuwasema Yanga hawana habari na sisi. Unawaita washamba na wamekutia bao 5? Kabla ya press msemaji anakunywaga nini? Yule jamaa huwa wanamchanganyia vitu, tunaonekana sisi timu yetu sio wastaarabu.

“Sisi kila mwaka tunaishia robo fainali, Yanga ana uwezo wa kufika nusu fainali, akivuka tutafanyaje? Kati ya wewe nay eye nani mshamba? Tuwe tunaweka akiba ya maneno. Kama mtu ambaye akili zako ziko sawa huwezi kuviita vilabu vilivyofuzu ni washamba… ningekuwa karibu ningemzaba kibao nimweke akili sawa,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live